(Kocha wa Everton Frank Lampard akilalamika kwa muamuzi)
Msimamizi huyo wa waamuzi Mike Riley ameomba msamaha kwa mwenyekiti wa Everton Bill Kenwright na kocha Frank Lampard baada ya kukiri kwamba waliwanyima penalti mwisho wa wiki iliyopita, baada ya kiungo wa city Rodri kuucheza mpira wa mikono. Taarifa za jana Jumatatu ziliasema kwamba Everton iliwasilisha malalamiko rasmi kwa njia ya maandishi juu ya tukio hilo.

(Kiungo wa Manchester City Rodri akiucheza mpira kwa mkono)
The Toffees walionyesha kukasirishwa na kitendo hicho baada ya mchezo kumalizika kwa kupoteza kwa goli 1- 0 wakiwa nyumbani dhidi ya Manchester City Jumamosi iliyopita huku waamuzi wasaidizi wa uwanjani pamoja na wale wa njia ya picha za marudio VAR wakiamua kutokuidhinisha mkwaju wa penati baaya ya Rodri kuonekana akiucheza mpira kwa mkono katika eneo la hatari.


